MABADILIKO YA TABIA YA NCHI YATAJWA KUWA CHANZO CHA KUKAUSHA MABWAWA YA KUZALISHA UMEME

MABADILIKO YA TABIA YA NCHI YATAJWA KUWA CHANZO CHA KUKAUSHA MABWAWA YA KUZALISHA UMEME

Like
176
0
Wednesday, 18 November 2015
Local News

MABADILIKO ya Tabia Nchi, uharibifu wa vyanzo vya maji katika mito mbalimbali na uchepushaji wa maji kwa ajili ya shughuli za kilimo na ufugaji ni chanzo cha kukauka kwa mabwawa ya maji yanayotumika katika kuzalisha umeme.

 

Hayo yamesemwa jijini Dar es salaam na msemaji wa Wizara ya Nishati na Madini Bi. Badra Masoud alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ukaguzi wa wezi wa umeme nchini.

 

Akizungumzia hali ya umeme nchini, Badra amesema kuwa kwa sasa hakuna mgawo wowote unaoendelea kwani uzalishaji ni mzuri, kiasi cha umeme kinachopatikana sasa ni megawati 1500 wakati matumizi kwa siku ni megawati kati ya 800 na 900.

Comments are closed.