MABEDUI WAPATIWA URAIA WA KIUCHUMI COMORO

MABEDUI WAPATIWA URAIA WA KIUCHUMI COMORO

Like
433
0
Monday, 10 November 2014
Global News

MAELFU YA WATU wasiokuwa na Uraia wanaoishi nchini Kuwait,wanatarajia kupatiwa uraia katika visiwa vya Comoro vilivyoko katika bahari ya Hindi.Taarifa hiyo imetangazwa na serikali ya Kuwait .

Taarifa zaidi zimeeleza kuwa Watu wasiokuwa na uraia wanaojulikana kama “MABEDUI” watapatiwa kile kinachojulikana kama “Uraia wa kiuchumi”.

Naibu katibu wa Wizara ya mambo ya ndani ya Kuwait,Meja Jenerali MAZEN AL-JARRAH amesema Mpango huo unatarajiwa kuanza mara tu baada ya visiwa vya Comoro kufungua ofisi yake ya Ubalozi mjini Kuwait miezi michache ijayo.

Bidoon-men-protest-outside-parl

Comments are closed.