MACEDONIA KUFUNGUA MIPAKA KWA WAHAMIAJI

MACEDONIA KUFUNGUA MIPAKA KWA WAHAMIAJI

Like
228
0
Monday, 24 August 2015
Global News

MAELFU ya wahamiaji, wengi wao wakimbizi wa Syria, wamesafiri kupitia Macedonia na Serbia wakielekea Ulaya Magharibi.

Shirika la Umoja wa Mataifa linalowahudumia wakimbizi UNHCR limesema zaidi ya watu  elfu 7,000 wakiwemo wanaume, wanawake na watoto, walivuka mpaka na kuingia kusini mwa Serbia na Macedonia usiku wa kumkia jana Jumapili, huku wengi wakitarajiwa kuwasili.

Shirika hilo limesema jana limehakikishiwa na serikali ya Macedonia kwamba mipaka itakuwa wazi kwa wakimbizi wanaokimbia mizozo katika nchi zao.

Comments are closed.