MACHAFUKO BURUNDI: IDADI YA WAKIMBIZI YAONGEZEKA TANZANI

MACHAFUKO BURUNDI: IDADI YA WAKIMBIZI YAONGEZEKA TANZANI

Like
271
0
Thursday, 28 May 2015
Local News

IMEELEZWA kuwa kutokana na kitendo cha rais wa burundi pierre Nkurunziza kung’ang’ania madarakani na kusababisha machafuko ndani ya nchi hiyo, hali hiyo imechangia kwa kiasi kikubwa kuwepo kwa ongezeko la wakimbizi kutoka burundi Nchini Tanzania kwa kuwa ndiyo nchi jirani iliyopakana na nchi hiyo.

 

Wakizungumza na EFM katika kambi ya muda ya wakimbizi hao iliyopo mjini kigoma katika uwanja wa Lake Tanganyika,wakimbizi hao wameeleza kuwa chama tawala kinachoongozwa na rais Nkurunziza kimekuwa kikitishia hali ya usalama wa maisha ya wananchi endapo watabainika kuwa ni wafuasi wa vyama pinzani na hawafuati matakwa ya chama hicho.

Comments are closed.