IMEELEZWA kuwa zaidi ya raia laki 126,000 wa Burundi wamekimbilia nchini Tanzania tangu mwezi Aprili, 2015, kufuatia machafuko ya kisiasa nchini humo.
Huku tayari wakimbizi elfu 64,000 kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC) wakiwa tayari nchini.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ametoa dola za Marekani milioni 100, sawa na shilingi za Tanzania bilioni 220 kutoka katika Mfuko Mkuu wa Kushughulikia Dharura wa Umoja wa Mataifa -CERF kwa shughuli za misaada katika maeneo tisa yenye dharura duniani na yasiyo na fedha za kutosha. Tanzania imetengewa dola za Marekani milioni 11 Sawa na shilingi za Tanzania bilioni 24 kutoka katika kiasi hicho .