MACHAFUKO BURUNDI: RAIA 126000 WAKIMBILIA TANZANIA

MACHAFUKO BURUNDI: RAIA 126000 WAKIMBILIA TANZANIA

Like
225
0
Monday, 01 February 2016
Local News

IMEELEZWA kuwa zaidi ya raia laki 126,000 wa Burundi wamekimbilia nchini Tanzania tangu mwezi Aprili, 2015, kufuatia machafuko ya kisiasa nchini humo.

Huku tayari wakimbizi  elfu 64,000 kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC) wakiwa tayari nchini.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon  ametoa dola za Marekani milioni 100, sawa na shilingi za Tanzania bilioni 220 kutoka katika Mfuko Mkuu wa Kushughulikia Dharura wa Umoja wa Mataifa -CERF kwa shughuli za misaada katika maeneo tisa yenye dharura duniani na yasiyo na fedha za kutosha. Tanzania imetengewa dola za Marekani milioni 11 Sawa na shilingi za Tanzania bilioni 24 kutoka katika kiasi hicho .

Comments are closed.