MACHALI AITAKA SERIKALI KUHESHIMU MISINGI YA UTAWALA BORA

MACHALI AITAKA SERIKALI KUHESHIMU MISINGI YA UTAWALA BORA

Like
383
0
Friday, 21 November 2014
Local News

KAMBI RASMI ya Upinzani Bungeni imeishauri serikali kuwashirikisha kikamilifu wananchi masuala mbalimbali muhimu ili wawe na uelewa wa kutosha kuhusu masuala hayo kabla ya kuyaridhia moja kwa moja.

Ushauri huo umetolewa leo Bungeni mjini Dodoma na msemaji wa kambi ya upinzani kupitia wizara ya uchukuzi mheshimiwa MOSES MACHALI wakati akichangia muswada wa azimio la bunge kuridhia itifaki ya kuzuia vitendo vya uharamia dhidi ya miundombinu ya kudumu iliyojengwa chini ya bahari ya mwambao wa bara ya mwaka 1988 iliyowasilishwa na Waziri wa Uchukuzi dokta HARRISON MWAKYEMBE.

Mbali na ushauri huo Mheshimiwa MACHALI amesema kuwa ili kufanikisha itifaki hiyo ya kuzuia vitendo vya uharamia wa miundombinu ni vyema kwa viongozi kuzingatia na kuheshimu misingi ya utawala bora.

 

Comments are closed.