MADEREVA WA MABASI NA MALORI YA MIZIGO WAPANGA KUFANYA MGOMO MKUBWA

MADEREVA WA MABASI NA MALORI YA MIZIGO WAPANGA KUFANYA MGOMO MKUBWA

Like
949
0
Wednesday, 08 April 2015
Local News

MADEREVA wa mabasi ya abiria na malori ya mizigo nchini,wako kwenye mikakati mizito ya kuingia kwenye mgomo mkubwa, unaotarajiwa kuanza Ijumaa.

Makakati huo unalenga kushinikiza Serikali kuingilia kati na kuyapatia ufumbuzi wa kudumu malalamiko yao dhidi ya Mamlaka za serikali, ikiwemo kikosi cha usalama Barabarani na Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Majini na nchi Kavu-SUMATRA.

Aidha madereva hao wameomba kukutana na Waziri wa Uchukuzi,SAMWEL SITTA,ili kuwasilisha malalamiko yao na kwamba ombi hilo likishindikana,hakutakuwa na maongezi zaidi ya kuanzisha mgomo usiokuwa na kikomo.

Comments are closed.