MADEREVA WA MAGARI YA MIZIGO WAITAKA TANROADS IONGEZE MIZANI

MADEREVA WA MAGARI YA MIZIGO WAITAKA TANROADS IONGEZE MIZANI

Like
450
0
Thursday, 02 April 2015
Local News

MADEREVA wa magari makubwa ya mizigo wamemtaka wakala wa Barabara Tanzania-TANROADS,kujenga mizani mingi kama iliyopo eneo la Vigwaza,Bagamoyo mkoani Pwani,huku wakisisitiza kuwa,itapunguza foleni na rushwa.

Wakizungumza na Efm,baadhi ya madereva ambao walikuwa wakielekea nchini Zambia,wamesema tangu mizani hiyo ianze ,kazi ya kupima imekuwa na ufanisi mkubwa tofauti na mizani ya Kibaha.

Akizungumzia Mzani huo,Dereva HUSSEIN AMOUR amesema kuwa,kwa sasa hakuna ucheleweshaji wa kupima,jambo ambalo halikuwepo hapo awali.

Comments are closed.