MADEREVA WA UDA WAWEKA MGOMO

MADEREVA WA UDA WAWEKA MGOMO

Like
441
0
Friday, 14 November 2014
Local News

Madereva wa UDA wamegoma kuingia barabarani kutokana na uongozi wa UDA kuweka kima cha juu cha kupeleka mapato kwa viongozi. Kampuni UDA wao wanaitaji laki 205000/= na madereva wao wanaitaji kupunguziwa walete sh 170000 kutokana na kuongezeka kwa magari ya UDA hivyo biashara imekuwa ngumu tofauti na awali.

Uongozi wa uda ulituma meseji hii,m  kwa wafanyakazi wa uda wote.              

Habari kwa madereva wote wa uda,kutokana na kikao cha uongozi wa UDA na uongozi wa madereva wa UDA,maamuzi yafuatayo yametolewa.

Hesabu itabaki kuwa 205000/= kwa hiyo kama hautakubaliana na hesabu hiyo njoo kesho asubuhi saa 2:30 asubuhi aandika barua ya kuacha kazi na kama utakubaliana na hesabu ya 205000/= njoo alfajili kuanzia saa 10:30 kwa ajili ya kuamsha gari.

By utawala-UDA.

-Madereva wameelezea kuhusu mgomo wao

Msemaji wa kampuni ya UDA –GEORGE MAZIKU alishindwa kutoa ushirikiano kutosha… …

-Ila Meneja wa Mawasiliano wa SUMATRA -DAVID MZIRAY anaelezea juu ya mwendelezo wa kuweka mistari kwenye mabasi ya UDA…

Comments are closed.