WAKAZI wa Manispaa ya Morogoro leo wamelazimika kutembea kwa miguu na wengine kutumia magari ya mizigo pamoja na pikipiki kwenda kazini huku wanafunzi wakibaki katika vituo vya daladala baada ya madereva kugoma wakishinikiza jeshi la polisi kuwaachia huru baadhi ya madereva wanaoshikiliwa kwa siku sita mfululizo kutokana na makosa ya usalama barabarani.
Wakizungumza na Efm, katika vituo mbalimbali vya daladala mkoani humo, wakiwemo wanafunzi na wanachi waliokwama kufika sehemu mbalimbali wamelalamikia serikali kushindwa kudhibiti mambo kama hayo ambayo yanaleta kero na usumbufu kwa raia ambapo mgomo huo umeathiri mambo mengi ikiwa ni pamoja na wanafunzi wa sekondari waliokuwa kwenye mitihani ya majaribio.