MADIWANI WAAPISHWA TEMEKE

MADIWANI WAAPISHWA TEMEKE

Like
381
0
Friday, 11 December 2015
Local News

UONGOZI  wa Manispaa ya Temeke jijini Dar es salaam umekamilisha zoezi la kuapishwa kwa Madiwani wa Wilaya hiyo,  zoezi ambalo limefatiwa na upigaji kura za kupata Meya pamoja na Naibu Meya wa Manispaa hiyo.

 

Katika zoezi hilo ambalo limefanyika siku ya jana Addallah Chaulembo wa CCM amefanikiwa kushinda nafasi ya kuwa Meya wa Manispaa ya Temeke wakati Hassan Feisal wa CCM amechaguliwa kuwa Naibu Meya.

 

Mara baada ya kuchaguliwa Meya wa Manispaa ya Temeke Abdallah Chaulembo amesema wananchi wa Manispaa hiyo watarajie mambo makubwa katika maendeleo ya Manispaa hiyo huku akiwataka Madiwani wa vyama vyote kuwaunga mkono.

Comments are closed.