MAELEZO YA PICHA TEGETA

MAELEZO YA PICHA TEGETA

Like
385
0
Monday, 26 October 2015
Entertanment

SHANGWE za muziki mnene wa 93.7 EFM  bado zinaendele.Ijumaa iliyopita

ilikuwa zamu ya wakazi wa Tegeta . Burudani ya aina yake  ikiongozwa na

timu nzima ya EFM ilishushwa ndani ya kimori high way park Tegeta , huku

wakazi wa Tegeta wakikutana ana kwa ana na watangazaji na RDJ’s wa

93.7EFM.

Burudani ilianza na kabumbu kati ya EFM na Boko beach veteran katika

uwanja wa boko beach  ambapo EFM waliibuka na ushindi mabao matatu  huku

Boko beach veteran wakiambulia sifuri.

Muziki mnene bado unaendelea, nawaambia wasikilzaji wetu ambao

hatujawafikia wawe wavumilivu na wajiandae kwa kuwa tutawafikia kuwapatia

burudani ya aina yake, alisema Dennis Ssebo mkuu wa idara ya mawasiliano na

mahusiano EFM.

unnamed

Wafanyakazi wa EFM waliojumuika na mashabiki uwanjani

unnamed3

Mashabiki waliojitokeza uwanjani kushudia mechi hiyo.

unnamed2

Timu ya EFM na boko beach veteran katika picha ya pamoja kabla ya

mechi kuanza.

unnamed4

Nyomi ya wakazi wa tegeta waliojitokeza kimori highway park

Tegeta.

 

 

Comments are closed.