MAELFU WALIOKWAMA KUTOKANA NA MAFURIKO WAOKOLEWA MALAWI

MAELFU WALIOKWAMA KUTOKANA NA MAFURIKO WAOKOLEWA MALAWI

Like
239
0
Monday, 19 January 2015
Global News

UTAWALA nchini Malawi umesema kuwa umewaokoa maelfu ya watu ambao walikuwa wamekwama kutokana na mafuriko ambayo yameikumba nchi hiyo.

Wanajeshi walitumia mashua na ndege za helikopta kuwahamisha watu kwenda maeneo yaliyoinuka kufuatia kuharibiwa kwa barabara na madaraja.

Takriban watu 200 wameripotiwa kufariki dunia huku wengine laki 2 wakilazimika kuhama makazi yao.

 

Comments are closed.