MAELFU WAMLAKI PAPA FRANCIS EQUADOR

MAELFU WAMLAKI PAPA FRANCIS EQUADOR

Like
190
0
Monday, 06 July 2015
Global News

KIONGOZI wa kanisa Katoliki duniani Papa Francis yuko nchini Equador ambako alilakiwa na maelfu ya watu waliojitokeza barabarani jana jioni.

Baba Mtakatifu Francis anatarajiwa kutoa hotuba 22 wakati wa ziara yake ya siku nane ambayo pia itamfikisha Bolivia na Paraguay.

Mataifa hayo matatu ni miongoni mwa mataifa maskini kabisa katika bara la Amerika ya Kusini na Papa Francis mwenye umri wa miaka 78 mzaliwa wa Argentina, amesema ataangazia mahitaji ya watoto, wazee, wagonjwa na wafungwa.

Comments are closed.