Maelfu ya wakimbizi kutoka Jamhuri ya Afrika ya Kati waliokimbilia Jamhuri ya Kidmekorasia ya Congo sasa wanakumbwa na balaa la njaa.
Shirika la Madaktari Wasio na Mipaka, MSF, limesema wakimbizi hao walioko kaskazini mashariki mwa Congo wanakabiliwa na utapiamlo kwani hawapati chakula na maji ya kutosha na wanategemea tu wahisani kuwapatia mahitaji ya msingi.
Katika kipindi cha wiki moja iliyopita, MSF imeshuhudia watoto kumi wakilazwa hospitalini kutokana na utapiamlo.