MAFUNZO YAKUKABILIANA NA MIONZI YA NYUKLIA YATOLEWA NCHINI

MAFUNZO YAKUKABILIANA NA MIONZI YA NYUKLIA YATOLEWA NCHINI

Like
227
0
Tuesday, 08 December 2015
Local News

TUME ya Nguvu za Atomiki, Tanzania kwa kushirikiana na Shirika la Nguvu za Atomiki Duniani wanaendeshesha mafunzo ya namna ya kukabilina na matukio ya mionzi hatari yenye lengo la kutoa mwongozo jinsi ya kukabiliana na majanga yanayoweza kusababishwa na mionzi hatari ya nyuklia.

Akifungua mafunzo hayo Jijini Arusha, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomiki nchini dokta Mwijarubi Nyaruba amesema kutokana na kukua kwa kasi kwa teknolojia duniani ni muhimu kwa nchi wanachama wa shirika la nguvu za atomiki duniani kuendelea kutoa mafunzo jinsi ya kukabiliana na majanga yanayotokana na nguvu hizo.

Aidha dokta Nyaruba amesema kuwa kutokana na ongezeko la vitendo vya ugaidi duniani ni lazima kujiimarisha ili kuweza kulinda vyanzo vyote vya mionzi vinavyotumika sehemu mbalimbali ikiwemo hospitalini na viwandani.

Comments are closed.