MAGAIDI KUCHUKULIWA HATUA UFARANSA

MAGAIDI KUCHUKULIWA HATUA UFARANSA

Like
268
0
Thursday, 15 January 2015
Global News

SERIKALI ya Ufaransa imewataka waendesha mashtaka kuchukua hatua thabiti dhidi ya Watu waliotekeleza vitendo vya kigaidi.Waziri wa Sheria nchini humo,Christiane Taubira amesema maneno au vitendo vya chuki dhidi ya mwingine vinavyotolewa kwa sababu ya imani ya dini vikomeshwe.

Zaidi ya Kesi 50 zimefunguliwa dhidi ya Watu wanaotuhumiwa kuhusika na shambulio la kigaidi wiki iliyopita na kusababisha watu 17 kupoteza maisha.

Wakati hayo yakijiri,kumekuwa na mapokeo hasi kwa Waumini wa kiislamu baada ya kuchapishwa kwa Jarida lenye kibonzo kinachomuonyesha Mtume Mohamad akiomboleza. Kiongozi mmoja wa kidini na Mufti wa Jerusalem ameita chapisho la jana kuwa ni tusi jingine kwa waislam.

 

 

Comments are closed.