MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA YASHIKA KASI KATIKA NCHI ZINAZOENDELEA

MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA YASHIKA KASI KATIKA NCHI ZINAZOENDELEA

Like
197
0
Wednesday, 01 July 2015
Local News

IMEELEZWA kuwa, Magonjwa yasiyoambukiza kama vile kansa, kisukari na shinikizo la damu, yameonesha kushika kasi katika nchi zinazoendelea hususani nchi ambazo zinauchumi mdogo zaidi ikiwemoTanzania.

Hayo yamesemwa leo na Kaimu Mkurugenzi wa Tiba Wizara ya Afya Dokta CHARLES MASSAMBU alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari baada ya ufunguzi wa semina iliyoandaliwa na Wizara hiyo ambayo imehusisha Sekta mbalimbali yenye lengo la kujadili namna ya kuthibiti na kuzuia magonjwa yasiyokuwa ya kuambukiza nchini.

 

Comments are closed.