MAGUFULI ACHUKUA FOMU NEC KUWANIA URAIS

MAGUFULI ACHUKUA FOMU NEC KUWANIA URAIS

Like
199
0
Tuesday, 04 August 2015
Local News

Mgombea wa nafasi ya Urais kupitia chama cha mapinduzi –CCM-dokta JOHN MAGUFULI leo amechukua fomu ya kugombea nafasi hiyo katika ofisi ya uchaguzi-NEC.

Akizungumza mbele ya mamia ya wanachama na wananchi mbalimbali waliojitokeza kwaajili ya kumpa salam dokta Magufuli amewahakikishia watanzania kuwa hatowaangusha endapo atapewa ridhaa na wananchi kuliongoza Taifa.

Awali akimkaribisha dokta Magufuli mwenyekiti wa chama hicho Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania dokta Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa kwa kipindi kirefu chama hicho kimeendelea kutoa viongozi wanaojali utawala bora hali iliyosababisha apewe shahada ya sheria nchini Australia.

Comments are closed.