MAGUFULI ATENGUA UTEUZI WA MKUU WA MKOA WA SHINYANGA MAMA ANNA KILANGO MALECELLA

MAGUFULI ATENGUA UTEUZI WA MKUU WA MKOA WA SHINYANGA MAMA ANNA KILANGO MALECELLA

Like
350
0
Monday, 11 April 2016
Local News

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dokta John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mama Anna Kilango Malecella kwa kubaini kuwa alimwambia uwongo kuwa Mkoa wake hauna wafanyakazi hewa wakati wapo wengi.

 

Rais Magufuli amesema kwamba hakuamini kwamba kuna mkoa ambao hauna wafanyakazi hewa, hivyo akatuma kikosi kazi ambacho hadi usiku wa kuamkia leo kimebaini kuwepo kwa wafanyakazi hewa 45 mkoani Shinyanya.

 

Akizungumza baada ya kupokea Ripoti ya TAKUKURU kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru Valentino Mlowola Rais Magufuli amesema amesikitishwa na kauli ya Mama Malecela ambaye bila shaka alikuwa amepata ushauri mbaya kutoka kwa watendaji wake.

Comments are closed.