MAGUFULI KUCHUKUA FOMU NEC LEO

MAGUFULI KUCHUKUA FOMU NEC LEO

Like
222
0
Tuesday, 04 August 2015
Local News

MGOMBEA wa nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi-CCM dokta JOHN POMBE MAGUFULI leo anatarajia kuchukua fomu ya kugombea nafasi hiyo katika ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi-NEC.

Katika Zoezi la uchukuaji wa fomu pia Mheshimiwa MAGUFULI ataambatana na mgombea mwenza wa chama hicho kutoka Zanzibar SAMIA SULUHU HASSANI.

Mbali na kuchukua fomu mheshimiwa Magufuli atapata nafasi ya kukutana na wadau wa siasa wakiwemo wananchi katika ofisi ndogo za CCM ili aweze kuwapa neno la shukrani.

Comments are closed.