MAGUFULI KUCHUKUA FOMU YA KUWANIA URAIS NEC KESHO

MAGUFULI KUCHUKUA FOMU YA KUWANIA URAIS NEC KESHO

Like
193
0
Monday, 03 August 2015
Local News

MGOMBEA Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi-CCM JOHN POMBE MAGUFULI kesho anatarajia kuchukua fomu ya kugombea nafasi hiyo katika ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi-NEC.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam leo Katibu Mwenezi wa Chama cha Mapinduzi NAPE NNAUYE amesema kuwa Mheshimiwa MAGUFULI katika msafara wake kuelekea NEC ataambatana na mgombea mwenza kutoka Zanzibar mheshimiwa SAMIA SULUHU HASSANI.

Comments are closed.