MAGUFULI KUZUNGUMZA NA WANANCHI DSM LEO

MAGUFULI KUZUNGUMZA NA WANANCHI DSM LEO

Like
210
0
Tuesday, 14 July 2015
Local News

MGOMBEA wa Nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi-CCM-dokta John Magufuli anatarajiwa kuwahutubia wananchi wa mkoa wa Dar es salaam ikiwa ni sehemu ya kutambulishwa kwake.

Akizungumzia suala hilo katibu wa siasa na Uenezi wa chama hicho Mkoani hapa Juma Simba amesema kuwa dokta Magufuli atawahutubia wananchi katika viwanja vya Mbagala Zakheim, hotuba itakayolenga kuonesha vipaumbele vya chama katika kipindi kijacho cha uongozi.

Dokta Magufuli alipitishwa kuwa mgombea wa nafasi hiyo kupitia –ccm- baada ya kupata ushindi wa kura 2104 ikiwa ni sawa na asilimia 87.1 kati ya kura 2416 zilizopigwa na wajumbe wa mkutano mkuu wa chama hicho.

Comments are closed.