MAHAKAMA AFRIKA YA KATI YAFUTA MATOKEO YA UBUNGE

MAHAKAMA AFRIKA YA KATI YAFUTA MATOKEO YA UBUNGE

Like
219
0
Tuesday, 26 January 2016
Global News

MAHAKAMA ya kikatiba nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati imefuta matokeo yote ya uchaguzi wa ubunge kutokana na kasoro nyingi zilizojitokeza wakati wa uchaguzi.

Mbali na hayo Mahakama hiyo pia imeidhinisha matokeo ya uchaguzi wa urais, ambao ulifanyika katika kipindi cha mwezi mmoja uliopita.

 

Hata hivyo imethibitisha kwamba mawaziri wakuu wa zamani Anicet- Dologuele na Faustin Touadere watakutana kwenye duru ya pili ya uchaguzi Februari 7 mwaka huu.

Comments are closed.