UMOJA wa Afrika umesema mahakama maalumu itaundwa kwa ajili ya kuwashitaki washukiwa wa makosa ya uhalifu wa kivita nchini Sudani kusini ambapo imekumbwa na mzozo mkubwa tangu mwaka 2013.
Hatua hii inalenga kuunga mkono hatua ya Afrika kushughulikia migogoro yao wenyewe.
Uundwaji wa mahakama ni sehemu ya makubaliano ya Rais Salva Kiir na Kiongozi wa waasi, Riek Machar yaliyotiwa saini baada ya kuwepo shinikizo kutoka kwa viongozi wa kikanda.