MAHUJAJI KUKUSANYIKA LEO KATIKA MLIMA ARAFA

MAHUJAJI KUKUSANYIKA LEO KATIKA MLIMA ARAFA

Like
488
0
Wednesday, 23 September 2015
Global News

MAHUJAJI kutoka duniani kote wameanza kukusanyika leo hii katika mlima wa Arafat nchini Saudi Arabia kwa kisimamo cha siku nzima ambacho ndio kilele cha ibada ya Hijja inayofanyika kila mwaka.

Takriban mahujaji milioni 2 wanakusanyika bega kwa bega kwa siku nzima na Wengi wameonekana wakiwa wamenyanyua mikono yao juu huku wakimuomba msamaha Mwenyezi Mungu kwa makosa yao na ya jamaa zao.

Siku kama ya leo miaka 1,400 iliyopita, Mtume Muhammad alitoa khutba yake ya mwisho katika mlima huwo wakati wa Hijja na kuwatolea wito Waisilamu juu ya usawa na kuwataka waungane.

Comments are closed.