Maisha ya wengi yako hatarini kutokana na maafa ya kimbunga

Maisha ya wengi yako hatarini kutokana na maafa ya kimbunga

Like
740
0
Tuesday, 30 April 2019
Global News

Msumbiji inahitaji misaada ya haraka kuokoa maisha ya walioathirika na kimbunga Kenneth, shirika la msaada limesema.

Huku shirika la ‘Save the Children’ limesema hali waliokuwa nayo watu wa Msumbiji inatishia usalama wa maisha yao hivyo ni muhimu misaada zaidi itolewe.

Umoja wa mataifa umetoa kiasi cha fedha cha dola milioni 13 ili ziweze kuwasaidia wahanga wa kimbunga wa Msumbiji na Comoro kwa ajili ya chakula, maji na kurekebisha miundo mbinu.

Idadi ya vifo vilivyosababishwa na kimbunga , magharibi mwa Msumbiji vimefika 38 na vifo vingine vinatarajiwa kutokea, utawala umebainisha.

Kwa sasa wafanyakazi wa mashirika ya msaada yanahangaika kufika katika maeneo ambayo yameathirika zaidi na kimbunga.

Mvua kubwa ilipiga kusini mwa Afrika mwishoni mwa wiki iliyoambatana na upepo mkali uliovuma kwa kilomita 220 kwa saa, na kusababisha zaidi ya maelfu ya makazi ya watu kuharibika.

Kwa sasa mvua si kubwa sana ingawa bado inaendelea kunyesha.

Mamlaka ya hali ya hewa inatabiri kuwa mvua hizi zitapiga mara mbili kama ilivyotokea kwenye kimbunga cha Idai ambacho kilitokea mwezi uliopita na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 900 katika maeneo ya kusini mwa Msumbiji, Malawi na Zimbabwe.

Afisa wa masuala ya misaada kwa binadamu kutoka Umoja wa mataifa anasema hatari za mafuriko ambayo yamesababishwa na kimbunga Kenneth zinatarajia kuendelea mpaka mwishoni mwa msimu wa mvua ambapo kiwango cha maji kwenye mito kitakuwa juu.

Tayari mji wa Pemba na Cabo Delgado umeathirika na mvua kubwa na mafuriko.

Kipi kipya?

Wafanyakazi wa shirika la msaada wanajaribu kupeleka dawa na kusambaza chakula kabla mvua nyingine kubwa haijaja.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kitengo cha taifa cha kukabiliana na majanga nchini humo, wamesema watu 38 wamefariki kutokana na kimbunga Keneth huku makazi 35,000 yameharibiwa na mvua.

Mtandao wa kujitegemea wa ‘O Pais’ umeripiti kuwa watu wengine watano wamefariki baada ya nyumba za Pemba kuanguka siku ya jumapili ingawa bado serikali haijathibitisha idadi ya vifo hivyo.

Watu laki mbili wapo hatarini Pemba peke yake, Ocha ilitoa angalizo.

Lakini kufika katika maeneo hayo hatari imekuwa kazi ngumu kwa wasaidizi kufanikiwa kufikia.

“Tumefanikiwa kutuma ndege moja kwa msaada wa shirika la chakula duniani ili kusambaza mchele na biskuti na vitu vingine ambavyo sio vyakula,

Lakini hali ya hewa imekuwa ikibadilika haraka sana na kuathiri operesheni hiyo ya kutoa misaada. Mvua zinaendelea kunyesha na walishindwa kutuma ndege nyingine”, Bwana Abreu aliiambia AFP

Kimbunga cha kitropiki huwa inatokea katika sehemu ya bahari ya hindi na huwa nadra kutokea.

Hata hivyo kwa mujibu wa mwandishi wa mazingira wa BBC ,Matt McGrath,Kimbunga Idai kilikuwa cha saba kupiga katika bahari hindi msimu ambao kilikuwa kimepiga mwezi achi.

Hii ni zaidi ya mara mbili ya kiwango cha kawaida kwa mwaka.

Kitu ambacho sio cha kawaida, licha ya kuwa kimbunga Idai na Kenneth vimepiga kwa mfululizo.

Kwa mujibu wa mamlaka ya hali ya hewa duniani imesema, kimbunga hiki kilichotokea Msumbiji kimevunja rekodi kwa sababu haijawahi kutokea kupiga mara mbili katika msimu mmoja.

Si hali ya kawaida kimbunga kuonekana katika maeneo haya na vilipungua kutokea yapata miongo saba iliyopita.

Lakini ni mapema sana au ni mfano mdogo kusema kuwa mabadiliko ya tabia nchi ndio yamesababisha mabadiliko haya.

Wataalamu wameainisha kuwa dhoruba hii inahusishwa na mabadiliko ya tabia nchi.

cc;BBSswahili

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *