MAJALIWA AIPIGANIA NAMUNGO FC YA JIMBONI KWAKE IPANDE LIGI KUU

MAJALIWA AIPIGANIA NAMUNGO FC YA JIMBONI KWAKE IPANDE LIGI KUU

Like
830
0
Sunday, 25 March 2018
Sports

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka wakazi wa wilaya ya Ruangwa washirikiane kuhakikisha ndoto ya timu yao ya mpira wa miguu ya Namungo FC ya kucheza ligi kuu inatimia.

Amesema timu hiyo limeupa mkoawa Lindi na wilaya hiyo heshima kubwa imepanda imepanda daraja kutoka ligi daraja la pili kwenda daraja la kwanza katika msimu wa 2018/2019.

Waziri Mkuu ameyasema leo (Jumamosi, Machi 24, 2018) wakati akizungumza na wakazi wa wilaya hiyo kwenye eneo la Namungo na kuwaomba waendelee kuisaidia timu hiyo ili iweze kupanda na kucheza ligi kuu.

Amesema daraja la kwanza linaushindani mkubwa zaidi, hivyo ameutaka uongozi wa timu hiyo kutumia siku 120 zilisalia kabla ya kuanza kwa ligi kwa kufanya maandalizi ya kuisuka timu hiyo kabla ya kuanza mashindano.

“Lazima timu yetu ya Namungo FC icheze daraja la kwanza kwa mafanikio makubwa, hivyo ni vema tukashirikiana kuhakikisha timu hiyo inafanikiwa ili ndoto ya kucheza ligi kuu itimie.”

Pia Waziri Mkuu amekagua eneo la ujenzi wa uwanja wa mpira wa miguu wilayani Ruangwa unaojengwa katika kitongoji cha Mtichi kata ya Nachingwea ambacho kinatarajiwa tumiwa na timu ya Namungo FC.

 

Awali, Mwenyekiti wa timu hiyo Bw. Hassan Kungu amesema Namungo FC imefanikiwa kupanda daraja na sasa inashiriki ligi daraja la kwanza na malengo yao ni kuhakikisha inafanya vizuri ili iweze kucheza ligi kuu.

“Mbali na mafanikio hayo, timu yetu ya Namungo FC inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa uwanja wenye viwango vya kuweza kucheza mashindano hao pamoja na chombo cha usafiri.”

Akizungumzia historia ya Namungo FC, Bw. Kungu amesema timu hiyo ambayo inamilikiwa na wachimbaji wa madini ya dhahabu katika eneo la Namungo wilayani Ruangwa ilianza 2009 kamasehemu ya mazoezi kwa wachimbaji hao mara wanapotoka kazini.

Comments are closed.