Katika harakati za maandalizi ya vikosi vya timu za mataifa 16 kutoka katika bara la afrika kuelekea kunako michuano mikubwa yakusaka taifa bingwa katika mchezo wa soka inayo taraji kuanza mnamo tarehe 17/01/2015.
Leo hii macho na masikio ya mashabiki walio wengi yanataka kusikia ama kuona ni taifa gani litaibuka kidedea katika michuano hiyo? Tutazame ubora na mafanikio ya timu mojamoja ambapo kwa sasa machoyetu yanaitazama timu ya taifa ya CONGO DRC ikiwa katika kundi “B” likiongozwa na Zambia,Tunisia na Cape Verde Island.
Kikosi cha timu ya taifa CONGO DRC almaarufu(the leopards) kimetangaza kikosi cha wachezaji 24 pamoja kiongozi wa wachezaji hao YOUSSOF MULUMBU anaekipiga kunako klabu ya West Brom Wich Albion inayo shiriki ligi kuu nchini uingereza.
Wachezaji tegemezi wa CONGO DRC ni mlinda mlango ROBERT KIDIABAwa Tp mazembe ,kiungo MIALA NKULUKUTU wa Tp mazembe YOUSSOF MULUMBU wa West Brom Wich, CEDRIC MAKIADI Weder Bremen,washambuliaji ni TRESOR MPUTU mazembe na LELO MBELE wa Petro Atletico
Kocha wa timu hiyo ni FLORENT IKWANGE IBENGE ambaye ni mzawa wanchi hiyo, IBENGE amesha wahi kuvinoa vilabu mbali mbali ikiwemo klabu ya SHANGHAI SHENHUA LIANSHENG inayo shiriki ligi kuu ya nchini china.
IBENGE mara ya kwanza kukiongoza kikosi cha CONGO DRC ilikua mwaka 2008-2009 katika harakati za kuwania kufuzu katika michuano ya kombe la mataifa Afrika na hatimaye kushindwa.
CONGO DRC imewahi kushiriki michuano hiyo mikubwa barani afrika mara 16 toka ilipo anzishwa mwaka 1957na imefika hatua ya robo fainal mara2,hatua ya nusu fainali mara 6 pamoja na kutwaa ubingwa mara 2 ikiwa ni mwaka 1968 na mwaka 1974.
Mchezo wa kwanza wa timu hiyo utapigwa saa moja usiku tarehe 18/01/2015 dhidi ya Zambia mchezo utakaochezwa katika uwanja wa ESTSDIO DE BATA wenye uwezo wa kubeba mashabiki 357,00 uliopo mjini BATA huko EQUTORIA GUINE.
|