MAKALA YA FLOYD MAYWEATHER JR

MAKALA YA FLOYD MAYWEATHER JR

Like
755
0
Friday, 23 January 2015
Slider

Kama ukipata nafasi ya kukutana na  kikundi cha mashabiki au wanamichezo duniani kote jaribu kuwauliza je ni mchezo gani unamashabiki wengi zaidi bilashaka watakujibu kuwa ni soka,

Mpiganaji maarufu duniani Michael Gerard Tyson yeye kwa upande wake aliulizwa na mmoja wa watangazaji wa kipindi cha michezo huko nchini marekani je unafikiri nimchezo gani mgumu zaidi kucheza kupita michezo yote? akajibu mpira wa miguu ni mchezo mgumu kuliko michezo yote.

Kwa upande wake mpiganaji maarufu duniani kwa sasa na nishabiki wa klabu ya Manchester united FLOYD MAYWEATHER JR almarufu kwa jina la (pretty boy money the best ever) labda anaweza kua na jibu sahihi la swali hilo.

MAYWEATHER amezaliwa tarehe 24 mwezi wa 2 mwaka1977 huko Grand RapidsMichigan na pambano lake la kwanza la mchezo huo ilikua tarehe 11 mwezi wa 10 mwaka 1996 alipo pigana na ROBERTO APODACA katika ukumbi wa  Texas Station Casino,huko Las VegasNevada  pambano  la ubingwa (BWAA) la raund 10 ambapo MYWEATHER alishinda kwa nock out katika raundi ya 2.

Mwaka 1993 baba wa mpiganaji huyo ROGER MYWEATHER    alihukumiwa kifungo     mara baada ya kukutwa na kosa la kuuza madawa ya kulevya huku akiwa ndiye mwalimu wa mtoto wake, MYWEATHER alikua akifundishwa na mjomba ake kwa kipindi chote ambacho baba yake hakuwepo uraiani.

Pambano lake la mwisho kucheza dhidi ya MARCOS MAIDANA lili kua la WBC MIDDLEWEIGHT ilikua tarehe13 mwezi 9 mwaka jana katika ukumbi wa grand hotel & casino uliopo las vegas Nevada ambapo MYWEATHER alishinda kwa point.

Jumla ya mapambano aliyocheza MYWEATHER ni 47 nakashinda yote 47 huku akishinda  26 kwa KO yani knockout, hajawahi kutoka sare wala kupigwa.

Masikio ya mashabiki wa mchezo huo kwa sasa wanatamani kuona mchezo mkali kati ya  MYWEATHER dhidi ya MANNY PACQUIAO unaotariwa kuchezwa mwezi wa 5 mwaka huu huko marekani . mchezo huo ulishawahi kupangwa uchezwe tarehe 5/12 /2009 lakini ilishindikana kutokana na sababu za hapa na pale kutoka kwa MYWEATHER.

Je unaweza kutueleza mchezo gani mgumu kucheza kuliko mingine?

Comments are closed.