MAKALA YA UCHAMBUZI KUELEKEKEA AFCON 2015 TAIFA LA EQUTORIAL GUINEA

MAKALA YA UCHAMBUZI KUELEKEKEA AFCON 2015 TAIFA LA EQUTORIAL GUINEA

Like
394
0
Thursday, 15 January 2015
Slider

Miezi michache iliyopita Shirikisho la soka barani afrika CAF linalo ongozwa na raisi wake Issa Hayatou lilikuwa katika wakati mgumu kutokana na taarifa iliyotolewa na walio kuwa waandaaji wa michuano hiyo mwaka huu MOROCO kujivua uwenyeji muda mchache kuelekea kuanza kwa michuano hiyo kwa kuogopa ugonjwa wa Ebola.

Shirikisho hilo kwa wakati tofauti likachagua mataifa ya GHANA,SOUTHAFRIKA na NIGERIA kuandaa michuano hiyo nayo yakatolea njee ombi hilo na kuibuka hali ya sintofahamu.

Mashabiki wengi walitahamaki kuona Raisi wa EQUTORIAL GUINEA Teodoro Obiang Nguema Mbasogo kutangaza yakua yupo tayari kuwa mwenyeji wa michuano hiyo mwakahuu bila ya kuogopa ugonjwa huo na CAF kupitisha ombi hilo.

EQUTORIAL GUINEA wakiwa wenyeji wa michuano hiyo mikubwa barani afrika kwa mara ya pili huku wakionekana kufanya maandalizi ya zimamoto kwa kuwa nyuma ya muda.

EQUTORIAL ipo katika kundi A ikiwa pamoja na BUKINAFASO,GABON na CONGO,Kikosi hicho kwa sasa kinanolewa na kocha ESTEBAN BECKER raia wa argentina ambaye pia anakinoa kikosi cha timu ya taifa hilo cha wanawake.

Wachezaji tegemezi wa timu hio ni capten Emilio Nsue anae kipiga katika klabu ya Middlesbrough ya nchini uingereza Aitor Embela,wa Malaga ya Hispania RAUL FABIANA wa olyimpic xativa ya Hispania.

Taifa hilo liliomba kuandaa michuano hiyo mwaka 2012 wakishirikiana na GABON huku EQUTORIAL ikiwa na viwanja viwili nakufanikiwa kujenga vingine viwili,viwanja hivyo ni ESTADIO DE BATA na kile cha ESTADIO DE MALABO.EQUTORIAL GUINEA imewahi kushiriki michuano hiyo mara 1 ikiwa wenyeji mwaka 2012 na ikaishia hatua ya robo fainal.

Ushindi mkubwa walio wahi kupata katika hitoria ya soka ni ule wa goli 3-0 dhidi ya Mauritania wakati wakiwania kufudhu katika michuano ya mwaka huu na hatimaye kushindwa,mchezo huo ulichezwa mwaka jana katika uwanja wa ESTADIO DE MALABO uliopo mjini malabo.

Mchezo wa kwanza wa timu hiyo utapigwa saa 12 jioni tarehe 17/01/2015 dhidi ya Congo ukiwa ni wa ufunguzi wa michuano hiyo mchezo utakaochezwa katika uwanja wa ESTSDIO DE BATA wenye uwezo wa kubeba mashabiki 357,00 uliopo mjini BATA huko EQUTORIA GUINE.

 

 

 

Comments are closed.