MAKAMANDA WA SUDANI KUSINI WAKUTANA ETHIOPIA

MAKAMANDA WA SUDANI KUSINI WAKUTANA ETHIOPIA

Like
250
0
Monday, 14 September 2015
Global News

MAKAMANDA wa kijeshi kutoka pande mbili zinazopigana nchini Sudan Kusini wanakutana mjini Addis Ababa nchini Ethiopia kujadili njia za kutekeleza makubaliano ya kusitisha vita.

Mkutano huo utazungumzia masuala yakiwemo kuondolewa vikosi kutoka vitani, kubuni maeneo yasiyo chini ya ulinzi wa kijeshi na kuondolewa kwa wanajeshi wa kigeni kutoka nchini humo.

Makubaliano ya amani yaliyotiwa sahihi mwezi uliopita yakiwa na lengo la kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe hayakutekelezwa huku pande zote zikilaumiwa kwa kukiuka makubaliano hayo.

Comments are closed.