MAKONDA AKABIDHIWA OFISI RASMI DARESALAAM

MAKONDA AKABIDHIWA OFISI RASMI DARESALAAM

Like
286
0
Tuesday, 29 March 2016
Local News

ALIYEKUWA mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Said Meck Sadick leo amemkabidhi rasmi ofisi mkuu wa mkoa mpya wa Dar es salaam Mheshimiwa Paul Makonda ambapo amemuomba Mkuu huyo mpya wa mkoa kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi ikiwemo afya na elimu.

Akizungumza mbele ya maofisa na watendaji mbalimbali ambao wamejitokeza kwa ajili ya kushuhudia makabidhiano hayo Mheshimiwa Sadick amesema licha ya yeye kufanya kazi kwa mafanikio bado kuna changamoto ambazo anaamini kutokana na uzoefu alionao mkuu huyo wa mkoa ajaye atafanikiwa kuzitatua.

Comments are closed.