MAKONDA: WANAWAKE CHANZO CHA UFISADI NCHINI

MAKONDA: WANAWAKE CHANZO CHA UFISADI NCHINI

Like
381
0
Monday, 16 May 2016
Local News

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema wanawake wamekuwa ni chanzo cha ufisadi nchini kutokana na kupokea zawadi zitokanazo na fedha za kifisadi.

Makonda aliyasema hayo wakati akizungumza na wananchi wa Kata ya Mnyamani Vingunguti Jijini Dar es Salaam jana katika mkutano wa kujadili namna ya kupata mikopo mbalimbali kutoka Benki ya Wananchi Dar es Salaam (DCB).

Makonda amewaambia wanawake hao kuwa hata katika suala la usafi linaanzia na malezi ya usafi ya akina mama kwa watoto tangu wakiwa wadogo jambo ambalo lingesaidia kupunguza changamoto zinazozikabili miji mbalimbali kwa kipindi hiki ambacho kuna changamoto ya usafi.

Comments are closed.