MAKONGORO NYERERE AKANUSHA TAARIFA ZA KIFO CHA MAMA YAKE

MAKONGORO NYERERE AKANUSHA TAARIFA ZA KIFO CHA MAMA YAKE

Like
433
0
Monday, 09 March 2015
Local News

MTOTO wa hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere, Makongoro Nyerere, amekanusha taarifa zilizotambaa Katika mitandao mbalimbali ya kijamii kuwa Mjane, Mama Maria Nyerere amefariki dunia.

Akizungumza na Efm kwa njia ya simu kutoka nchini Uganda, Mheshimiwa Makongoro amesema familia imesikitishwa na mtu aliyevumisha taarifa hizo, nakwamba mama yao ni mzima.

Hata hivyo amewataka Watanzania, kuacha tabia ya kuvumisha taarifa ambazo siyo za kweli kwani zinachangia upotoshaji kwa watu na badala yake kuwa na ufuatiliaji wa mambo kabla hawajaanza kuyajadili na kuyasambaza kwenye mitandao ya kijamii.

Comments are closed.