MAKTABA NCHINI KUJENGEWA UWEZO

MAKTABA NCHINI KUJENGEWA UWEZO

Like
227
0
Monday, 09 November 2015
Local News

BODI ya huduma za maktaba nchini-TLSB-imeanzisha mradi wa Maktaba kwa maendeleo wenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 630 ili kuzijengea uwezo wa utendaji kazi bora maktaba zote nchini.

Akizungumza katika mradi huo Mkurugenzi mkuu wa-TLSB-dokta Ali Mcharazo amesema Mradi huo ambao utatumia zaidi teknolojia ya habari na Mawasiliano-(Tehama)-kwa kutumia maktaba zinazohamishika, utawafikia walengwa moja kwa moja katika maeneo yao ya uzalishaji na kuwawezesha kupata taarifa muhimu za kuendeleza shughuli zao za kila siku.

Kwa Upande wao wakutubi wa Maktaba wamesema mradi huo utasaidia kuboresha huduma za maktaba ambazo mfumo wa uendeshaji wake awali ulikuwa ukikabiliwa na ushindani wa teknolojia.

Comments are closed.