MAKUNDI YA KIHUNI HUENDA YAKAMGAHARIMU CHRIS BROWN

MAKUNDI YA KIHUNI HUENDA YAKAMGAHARIMU CHRIS BROWN

Like
298
0
Thursday, 16 July 2015
Entertanment

Mwimbaji wa muziki wa r&b kutoka Marekani Chris Brown huenda akapoteza nafasi aliyoipigania kwa kipindi kirefu kuishi na binti yake Royalty.

Haya yanakuja mara baada ya nyumba yake kuvamiwa na kundi la waharifu hali aliyopelekea mama wa mtoto huyo kuwa na hofu ya kumpoteza mwanae atakapomuacha chini ya uangalizi wa Cris Brown kutokana na rekodi yake ya kujihusisha na makundi ya wahuni.

Nia Guzman anafikiria kuwa makundi hayo kwa sasa yanamrudia Cris na kumfanyia uhalifu hivyo ni hatari kwa maisha ya mtoto huyo

 

Tukio hili linakuja katika wakati ambao Cris Brown amefungua kesi ya madai kuomba kupewa kibali maalum kitachompa haki ya kimsingi kuhusika na malezi ya binti huyo huku sababu yake ya msingi ikiwa Nia anamkatalia kumtembelea mwanae, sasa huenda ikamuharibia kupatiwa nafasi hiyo

Comments are closed.