MAKUNDI YANAYOPIGANA SUDAN KUSINI YAKUTANA TANZANIA

MAKUNDI YANAYOPIGANA SUDAN KUSINI YAKUTANA TANZANIA

Like
242
0
Thursday, 22 January 2015
Global News

MAKUNDI yanayopingana nchini Sudan Kusini yamekusanyika nchini Tanzania kusaka jitihada mpya za kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa zaidi ya mwaka mmoja na kusababisha maelfu ya watu kuuawa.

Serikali ya Tanzania ambayo inasimamia mazungumzo ya Arusha kupitia chama tawala cha CCM nchini, imesema Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini na aliyekuwa naibu wake na sasa kuwa kiongozi wa waasi nchini humo Riek Machar walikutana Jumatano na kutiliana saini mkataba mpya wa amani.

Pande mbili hizo zilitiliana saini mkataba unaolenga kukiunganisha chama tawala cha the Sudan People’s Liberation Movement (SPLM), ili kumaliza uhasama uliojitokeza miongoni mwa viongozi wa chama hicho kilichopigania uhuru wa Sudan Kusini miaka mitatu iliyopita.

Comments are closed.