MALAYSIA YATOA WITO KUTOLEWA KWA TAARIFA JUU YA MABAKI YA NDEGE

MALAYSIA YATOA WITO KUTOLEWA KWA TAARIFA JUU YA MABAKI YA NDEGE

Like
200
0
Monday, 03 August 2015
Global News

MAAFISA nchini Malaysia wametoa wito kwa nchi zilizo karibu na kisiwa cha Reunion katika Bahari ya Hindi kusaidia kutoa habari zozote kuhusu mabaki ambayo huenda yanahusiana na ndege iliyotoweka ya Malaysia.

Wito huo umekuja baada ya kipande cha ubawa kupatikana katika kisiwa hicho magharibi mwa Bahari ya Hindi.

Kipande kipya cha mabaki kilichopatikana jana Jumapili katika kisiwa hicho kiligunduliwa kuwa ni ngazi ya kawaida ya nyumbani na wala hakihusiani na ndege hiyo ya Malaysia iliyotoweka mwaka mmoja uliopita.

Comments are closed.