MALI: HOTELI YASHAMBULIWA KATIKA MJI WA SEVARE

MALI: HOTELI YASHAMBULIWA KATIKA MJI WA SEVARE

Like
232
0
Friday, 07 August 2015
Global News

WATU waliojihami kwa kutumia bunduki wameshambulia zaidi ya hoteli mbili katika mji wa Sevare eneo la katikati ya nchini Mali.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo wameeleza kwamba watu hao waliokuwa  wakiendesha pikipiki wameingia katika eneo hilo na kuanza kufyatua risasi kwenye majengo hayo.

Imebainika kwamba ingawa Mji wa Sevare una kituo cha jeshi la anga pamoja na wanajeshi kadhaa wa kikosi cha umoja wa mataifa cha kulinda amani lakini bado matatizo kama hayo hujitokeza.

Comments are closed.