MALI YA SERIKALI YA ZIMBABWE YAPIGWA MNADA

MALI YA SERIKALI YA ZIMBABWE YAPIGWA MNADA

Like
226
0
Monday, 21 September 2015
Global News

IMEBAINIKA kuwa nyumba inayomilikiwa na serikali ya Zimbabwe imeuzwa kwa mwekezaji mmoja wa nchini Afrika kusini kwa kiasi cha dola za kimarekani laki mbili na Elfu themanini kupitia mnada.

Mnada huo umefanyika baada ya serikali hiyo kushindwa kwenye mzozo uliodumu kwa kipindi cha miaka mitano kati yake na shirika la kutetea haki za Waafrika nchini Afrika Kusini.

Shirika hilo liliitaka serikali ya Zimbabwe kulipa gharama ya kesi baada ya serikali hiyo kushindwa kwenye kesi iliyohusu mageuzi ya umiliki wa mashamba.

Comments are closed.