September 30 kwenye kipindi cha Ubaoni ilitoka ripoti ya mama mwenye watoto wanne akieleza jinsi alivyotelekezwa na mume wake na kupelekea yeye na watoto wake kukosa huduma muhimu za kimaisha.
Mama huyo aliyejitambulisha kwa jina la Frola Frank alitoa rai yake kwa watanzania wenye nia ya kumsaidia wajitokeze ili waweze kutoa misaada tofauti .
Moja ya watanzania ambae Hakutaka jina lake litwaje ni miongoni mwa watu walioguswa na mapito ya maisha ya mama huyu amejitolea kiasi cha shilingi laki nne kama sehemu ya msaada.
Unaweza kumchangia pia mama huyu kupitia namba hii 0713575718
RIPOTI YA LEO INAANDALIWA NA LIVINGSTONE MKOI MWANDISHI WA MATUKIO YA UCHUNGUZI E-FM
PICHA NI FROLA FRANK AKIKABIDHIWA FEDHA HIZO