MAMA NA BABA LISHE TANZANIA KUANZISHA UMOJA

MAMA NA BABA LISHE TANZANIA KUANZISHA UMOJA

Like
347
0
Friday, 13 November 2015
Local News

JUMUIYA ya Mama na Baba lishe Tanzania inatarajia kuunda umoja wao wenye malengo ya kutoa suluhisho la changamoto zinazowazunguka kwa kuanzisha Shirikisho la Saccos ili kutoa elimu mbalimbali za mkopo na ujasiliamali.

 

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam Mwenyekiti wa Jumuiya ya Mama lishe na Baba lishe Tanzania Ramadhan Mhonzu amesema kuwa malengo na madhumuni ya jumuiya hiyo ni kuunganisha Wadau mbalimbali ili kutoa nafasi za kulinda haki za ajira zao.

 

Kwa upande wake Katibu wa Jumuiya hiyo na Mama lishe wa Soko la Ilala Jane Nyanda amebainisha kuwa Jumuiya hiyo itakuwa chachu ya mabadiliko katika tasnia hiyo kwa vitendo kwa manufaa ya wote.

Comments are closed.