MAMA SALMA AMEWAOMBA WANANCHI KUIPIGIA KURA YA NDIO KATIBA PENDEKEZI

MAMA SALMA AMEWAOMBA WANANCHI KUIPIGIA KURA YA NDIO KATIBA PENDEKEZI

Like
268
0
Wednesday, 18 March 2015
Local News

MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Taifa -NEC ya Chama Cha Mapinduzi –CCM kupitia Wilaya ya Lindi mjini Mama SALMA KIKWETE, amewaomba wananchi kuipigia kura ya ndiyo Katiba Inayopendekezwa kwa kuwa ni bora na imezingatia mahitaji ya makundi yote ya jamii.

Mama KIKWETE ametoa ombi hilo wakati akiongea na Wananchi waliohudhuria mkutano wa hadhara uliofanyika  katika Tawi la Mikumbi Magharibi  Kata ya Wailes Wilayani humo.

Amesema Katiba inayopendekezwa ni ya Watanzania wote,na imegusa maeneo yote muhimu kwa Ustawi wa Wananchi, inazungumzia Haki za Wanawake, Wazee, Wavuvi, Watoto na watu wenye mahitaji maalum.

Comments are closed.