MAMA SALMA AWATAKA WAKAZI WA LINDI KUTOUZA MAENEO YA UFUKWE WA BAHARI

MAMA SALMA AWATAKA WAKAZI WA LINDI KUTOUZA MAENEO YA UFUKWE WA BAHARI

Like
294
0
Tuesday, 10 February 2015
Global News

MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia wilaya ya Lindi mjini Mama Salma Kikwete amewataka wakazi wa wilaya hiyo kutokubali kuuza maeneo ya ufukwe wa Bahari  ya Hindi kwa kiasi kidogo cha fedha  kwani thamani ya maeneo hayo ni kubwa.

Mama Kikwete ambaye ni Mke wa Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ametoa rai hiyo wakati akiongea  kwa nyakati tofauti  na viongozi wa Halmashauri kuu ya tawi ya Chama hicho  katika matawi ya Raha leo na Ufukoni yaliyopo katika kata ya Rahaleo wilayani humo.

Mama Salma Kikwete amesema hivi sasa kuna wageni wengi ambao wanaenda kwa wananchi na kununua maeneo ya ufukweni kwa bei ya chini lakini endapo wamiliki wa maeneo hayo watakuwa na subira watayauza  kwa bei kubwa  kwa kipindi cha  miaka michache ijayo.

 

Comments are closed.