MAMLAKA YA HALI YA HEWA YATOA TAHADHARI JUU YA KUWEPO KWA VIPINDI VYA MVUA KUBWA

MAMLAKA YA HALI YA HEWA YATOA TAHADHARI JUU YA KUWEPO KWA VIPINDI VYA MVUA KUBWA

Like
296
0
Monday, 19 January 2015
Local News

MAMLAKA ya Utabiri wa Hali ya Hewa Tanzania-TMA, imetoa tahadhari ya kuwepo kwa vipindi vya mvua kubwa inayozidi milimita 50 ndani ya saa 24 kati ya Januari 18 na 20 mwaka huu.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mamlaka hiyo kwa vyombo vya habari jijini Dar es salaam, maeneo yatakayoathirika na Mvua hiyo ni pamoja na Mikoa ya Ruvuma, Mtwara, Lindi, Morogoro, Pwani, Dar es salaam na Kisiwa cha Unguja.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa hali hiyo inatokana na kuimarika kwa mgandamizo mdogo wa hewa katika eneo la bahari ya Hindi Mashariki mwa Kisiwa cha Madagascar na hivyo kusababisha ongezeko la unyevunyevu kutoka misitu ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kuelekea katika maeneo hayo.

 

Comments are closed.