MAMLAKA YA VIWANJA VYA NDEGE YAANDAA MKAKATI WA KUPANUA NA KUBORESHA VIWANJA VYA NDEGE

MAMLAKA YA VIWANJA VYA NDEGE YAANDAA MKAKATI WA KUPANUA NA KUBORESHA VIWANJA VYA NDEGE

Like
347
0
Tuesday, 16 December 2014
Local News

MAMLAKA ya viwanja vya ndege Tanzania TAA imeandaa mkakati wa kupanua na kuboresha viwanja vyote vya ndege kwa kiwango cha lami jambo ambalo litakalosaidia kukua kwa uchumi wa nchi kupitia sekta ya usafiri wa anga.

Akizungumza jijini Dar es Salaam mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya ndege TAA Suleiman Suleiman amesema uboreshaji huo wa viwanja vya ndege kwa kiwango cha lami utasaidia kupunguza gharama za uendeshaji kwani ndege inapotua kwenye kiwanja cha tope gharama zake zinakuwa mara mbili zaidi tofautia na kwenye lami.

Suleiman ameeleza kuwa kwa kuanza kwa utekelezaji huo serikali imewekeza zaidi ya bilioni 105 katika kiwanja cha mwanza ikiwa ni moja ya mikakati ya kuhakikisha kiwanja hicho kinakidhi mahitaji ya eneo hilo la kanda ya ziwa na pia kuwa katika hadhi ya kimataifa kama kilivyo cha Julius Nyerere.

Aidha aliongeza kuwa ukarabati wa viwanja vyote vya ndege nchini utasaidia kupunguza gharama za usafiri huo wa anga kwani uendeshaji wake utashuka kwa kiwango kikubwa

Comments are closed.