Manchester City wamejiandaa kuanza mapambano dhidi ya Chelsea kuhusu huduma za mlinzi wa pembeni wa Leicester City Ben Chilwell, 23, baada ya kuonyesha kiwango murua akiwa kwa mbweha hao.
Napoli hawatapunguza bei ya beki wao raia wa Senegal Kalidou Koulibaly, 28, ambapo wanataka Pauni Milioni 100, haya yanakuja kipindi ambacho anahusishwa kujiunga na miamba kama Manchester United, Manchester City na Paris Saint Germain.
Manchester United na Real Madrid wanamchunguza mshambuliaji wa Inter Milan Lautaro Martinez 22, baada ya mazungumzo ya kujiunga na miamba ya Catalunya FC Barcelona kusimama kwa hivi sasa.
Kiungo wa Bosnia-Herzegovina na Juventus Miralem Pjanic, 30, amekataa ofa za kujiunga na Chelsea na Paris Saint Germain kwani anahitaji kujiunga na Barcelona.
Kiungo wa zamani wa Chelsea Michael Ballack ameukubali kwa asilimia 100 uamuzi wa klabu yake kumsajili mshambuliaji wa RB Leipzig Timo Werner, 24, kwani anaamini ataiga mapema mazingira ya soka la EPL.
Kiungo mshambuliaji wa Croatia na Fc Barcelona Ivan Rakitic, 32, anafikiria kuendelea kusalia klabuni hapo mpaka mwaka 2021 ambako kandarasi yake inatamatika.
Kiungo wa Paris St-Germain Ander Herrera, 30, amesema mshambuliaji wa Uruguay ambaye wanacheza pamoja Edinson Cavani, anatamani kucheza soka katika taifa la Hispania, Strika Cavani, 33, amekuwa akihusishwa kujiunga na Atletico Madrid.
Beki wa Manchester United Brandon Williams, 19, anawindwa na mawakala wawili juu ya kumsaini mlinzi huyo kisha wakawa wanamtafuti timu, masoko, usimamizi na masuala kama hayo.