MANCHESTER UNITED YAFIKIA MAKUBALIANO NA AS MONACO JUU YA ADA YA KUMSAJILI RADAMEL FALCAO

MANCHESTER UNITED YAFIKIA MAKUBALIANO NA AS MONACO JUU YA ADA YA KUMSAJILI RADAMEL FALCAO

Like
481
0
Friday, 31 October 2014
Slider

 

Klabu ya Manchester United imefikia makubaliano na klabu ya AS Monaco juu ya ada ya kumsajili moja kwa moja mshambuliaji wa kimataifa wa Colombia, Radamel Falcao.

Falcao alijiunga na klabu ya Manchester United kwa mkopo wa msimu mmoja akitokea AS Monaco kwa dau la euro million 8 huku kukiwa na kipengele kinachomruhusu kujiunga na mashetani wekundu mwisho wa mkataba huo.

Manchester United chini ya Ed-Woodward wamesema wapo teyari kulipa kiasi cha euro million 56 na mshahara wa kiasi cha euro laki tatu na elfu tano ili kupata huduma za EL TIGER.

Raia huyo wa Colombia bado anapigania nafasi katika kikosi cha kwanza kilicho chini ya Louis Van Gaal ambacho kimejaa mastaa kama Wayne Rooney, Robin Van Persie na Angel Di Maria.

radamel-falcao

RADAMEL FALCAO

Comments are closed.